Thursday, June 1, 2017

SAM FLAVIOUR KUACHIA NJOO ‘UJIONEE’

MSANII chipukizi kizazi kipya SAMWELI MWAILONDA a.k.a SAM FLAVOUR amesema kuwa hivi karibuni sasa ameeleza nguvu nyingi kwa kutoa nyimbo yake mpya ‘’ NJOO UJIONEE’’ambayo imempa mafanikio makubwa na kuomba sapoti kubwa kwa mashabiki wake Akizungumza na papaso la burudani SAM FLAVOUR ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake wa ‘NJOO UJIONEE’ alisema yeye na uongozi wake wana mipango endelevu na managementi yao zima ‘’Mipango yangu ya kuachia video ya NJOO UJIONEE’ ni kuweka mkakati wa kufanya kazi kwa wingi kwa sababu kila msanii anafanya vizuri kwa kuachia video nzuri na audio pia napenda kumshukuru sana Mungu kwa mafanikio makubwa . Mbali na swala la muziki pia anachukua masomo ya uandishi wa habari katika chuo cha habari (TSJ) ambapo ,masomo hayo haya mnyimi kabisa kufanya kazi yake ya kimuziki ambayo inamuingizia kipato ambacho kinamsaidia katika ulipaji ada.

No comments:

Post a Comment