Thursday, June 1, 2017
Kagera yafurahia pointi zao
THOMAS NG’ITU
WACHEZAJI wa timu ya Kagera Sugar wamefurahia kurudi kwa pointi zao ambazo walinyang’anywa na kamati ya masaa 72 baada ya kupewa tuhuma za kumchezesha mchezaji Mohammed Fakhi ambaye alisadikiwa kuwa ana kadi tatu za njano.
Akizungumza na Gazeti hili nahodha wa kikosi hicho George Kavila alisema kuwa wanafuraha kwa kurudi kwa pointi zao kwani ziliwafanya kuwachanganya kwa namna moja ama nyingine kisaikolojia lakini tulijiweka vizuri.
“Unajua katika sakata lile lilituumiz akwa namna moja ama nyingine kisaikolojia lakini viongozi wetu walizungumza na sisi katika suala hili na kukaa nao chini na kututengeneza kisaikolojia mpaka kufikia hivi sasa na kurudi kwa pointi hizi kumetuongezea ujasiri mkubwa katika kugombea nafasi za juu zaidi ya hapa”, alisema.
Naye straika wa timu hiyo Mbaraka Yusuph alisema kuwa Bodi ya Ligi inabidi iwe macho zaidi katika kufatilia ligi na makamisaa ambao wanakuwa wanatumwa wanabidi wawe makini katika kuandika ripoti zao sahihi.
“Vitu kama hivi vinaweza kabisa kuhepukika kwasababu kama bodi ya ligi wakiwa makini kuanzia makamisaa na marefa wao kivyovyote vile matatizo kama haya ni ngumu kutokea kwahiyo bodi ya ligi wanatakiwa wewe makini matatizo kama haya yasijirudie tena”, alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment